Video na Makala: Unyanyasaji wa wafanyakazi za ndani (Domestic workers)


   
SEKTA YA WAFANYAKAZI WA MAJUMBANI

Kazi za nyumbani hujumuisha kundi la kazi rasmi na zile zisizo rasmi ambapo mtu hufanya kazi akiwa nyumbani au karibu na nyumbani bila kwenda kwa mwajiri.kazi za nyumbani ni mmoja wa mfumo wa zamani ambao historia yake imeanzia kusini mwa Bara la Asia. Katika dunia ya utandawazi,kazi za nyumbani zimeimarika na kutoa faida hususani kwa kina mama ambao hawahitaji kwenda nje na hivyo kuunganisha kazi hizo na zile za kawaida zisizo na malipo wakati huo huo wakibakia nyumbani

Kazi za ndani ni moja ya kazi za zamani sana kwa mwanamke katika historia ya dunia.Kuna uhusiano mkubwa kati ya kazi za ndani na utumwa katika kipindi cha ukoloni ni moja ya sekta isiyo na usimamizi na isiyo na maendeleo kwasababu katika nchi nyingi sheria za kazi hazitumiki kwa wafanyakazi wa ndani.mwingine,kwa kufuzu kuwa mfanyakazi wa ndani ni lazima awe amefanya kazi za ndani katika makubaliano ya ajira
                            
 AINA ZA WAFANYAKAZI WA MAJUMBANI

Wafanyakazi wa ndani wamegawanyika katika makundi makubwa mawili [2].
1.      Wafanyakazi wanaoishi na waajiri wao majumbani.
2.      Wafanyakazi wa ndani waishio nje ya nyumba wanayofanyia kazi,yaani nje na mwajiri wake
anapoishi.

AINA YA KAZI ZA MAJUMBANI

Katika maazimio mapya yaliyokubaliwa na shirika la kazi la kimataifa  [ILO] mwezi Juni 2011 katika mkataba  [C 189] za kazi za ndani zimeeleza kuwa, kazi zifanyazo ndani ni pamoja na;

1.     Usafi
2.     Kufua
3.     Kupiga pasi
4.     Kupika
5.     Ulinzi wa nyumbani
6.     Uyaya(kulea watoto)
7.     Utunzaji wa mifugo ya familia
                                                      
SHERIA INAYOWALINDA WAFANYAKAZI WA NDANI

Wafanyakazi wa ndani wanalindwa na sheria ya ajira na mahusiano kazini namba 6 ya mwaka 2004.
mwaka 2011 juni Nchini Geneva Uswisi, shirika la kazi duniani [ILO] lilitoa mkataba wa kimataifa namba[C189] wa kazi zenye staha kwa wafanyakazi wa majumbani,ambao ndio mkataba unaopigwa kelele na wanaharakati wengi ili serikali wapeleke bungeni kujadiliwa kisha kupitishwa ili uwanze kutumika.






KIMA CHA MSHAHARA KWA MFANYAKAZI WA NDANI
Kima cha chini cha mfanyakazi wa ndani mpaka sasa ni sh.za kitanzania elfu 40,000.hiki ni kima cha mfanyakazi anaeishi kwa mwajiri wake.

WAJIBU WA WAFANYAKAZI WA MAJUMBANI
a)     Kuzifahamu haki zake za msingi
b)    Kufanya kazi kwa ufanisi na ustadi katika sehemu yake ya kazi.
c)     Kuheshimu,kuipenda,kuijali na kuithamini kazi yake.
d)    Kulinda na kuheshimu mali za mwajiri wake.
e)      kuwa mwangalizi wa familia pale ambapo mwajiri hayupo.

IDADI YA WAFANYAKAZI WA MAJUMBANI.

Kwa mujibu wa takwimu za shirika la kazi duniani kuna watu 5.2 milioni wanaofanya kazi za ndani barani Afrika.Hivyo kuwa bara la [3] kwa wingi wa wafanyakazi wa ndani baada ya Asia na Marekani kusini.Takwimu za ILO zinaonyesha kuwepo kwa wafanyakazi wa majumbani wapatao 53milioni duniani kote.Takwimu za mwaka 2008.

UMRI WA MTU KUFANYA KAZI ZA MAJUMBANI

Suala la umri katika ajira za majumbani limekuwa ni tatizo kwani watotot wamekuwa
wakifanyishwa hizi kazi kinyume na utaratibu.Imekuwa ni rahisi watoto kupatikana na
na kutumikishwa kwenye ajira hizi. Mtoto mdogo akipewa majukumu ya malezi ya mtoto.

Umri unaostahili kufanya kazi za majumbani ni miaka 18 na kuendelea.Wenye umri chini ya miaka 18 lakini si chini ya 15 wanaweza kuajiriwa kuwa wafanyakazi wa majumbani lakini kazi zao zisiwanyime elimu ya lazima, mafunzo ya ufundi ama kujiendeleza zaidi wale wanaoishi na waajiri wapewe kazi zenye staha waajiri wao  na zisiwe ngumu au nzito.

HAKI ZA MFANYAKAZI WA MAJUMBANI

  a)Maazimio mapya yanasisitiza upatikanaji wa haki za msingi kwa mfanyakazi wa ndani kama ilivyo kwa wafanyakazi wengine;
   b) Kulipwa mishahara/ujira wao kamili na kwa wakati
   c) Kufanya kazi kwa masaa yaliyowekwa kisheria.
   d) Kupata likizo ya mwaka/kupata matibabu yaliyo sahihi.
   e) Kufanya kazi katika mazingira ya afya na usalama.
   f) Haki ya kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii na vyama vya wafanya kazi.  
   g) Haki ya kutetewa haki zao za kupitia vyombo vya sheria


Comments