MAMBO 30
USIYOYAJUA KUHUSU MSITU WA AMAZON
1. Msitu wa Amazon ndio msitu mkubwa zaidi duniani unaopatikana
huko America kusini.
2. Kama ulifikiri msitu huu unapatikana Brazil pekee jibu ni hapana
msitu huu umegawanyika katika nchi tisa nchi hizo ni Blazil 60% peru 13%
colombia 10% na mataifa mengine kama Venezuela, Ecuador, bolvia, guyana,
suriname na France guiana.
3. Msitu huu una eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 5,500,000 (
Milioni 5) yani kwa ukubwa huu nchi ya TANZANIA iingie mara 6 kwenye msitu huo.
4. Kwa mujibu wa wanasayansi wa mimea msitu wa Amazon una umri wa
miaka zaidi ya million 55
5. Msitu wa Amazon unakadiriwa kuwa na miti billion 400 na aina
mbalimbali za miti zaidi ya 160,000 pia kuna miti ya matunda tofauti tofauti
elfu tatu katika msitu huo.
6. Mchanga wa jangwa la sahara hupeperushwa na upepo hupita juu ya
bahari Atlantic hadi katika msitu wa amazon ambako hurutubisha katika msitu
huo.
7. Katika msitu wa amazon kuna mto umekatisha mto huo unaitwa mto
amazon huu ndio mtu mkubwa zaidi duniani na unaingiza maji baharini mara 5 ya
mito mingine maajabu ya mto huu kuna muda haueleweki kuna kipindi unapeleka
maji kinyume badala ya maji kwenda mashariki yana kuwa yana toka mashariki
kwenda magharibi.
8.
Asilimia 20% ya oxygen iliyopo dunia inatengenezwa katika
msitu wa amazon acha hili pia zaidi ya asilimia 70% ya madawa ya kisasa
yana tengenezwa kwa kutumia miti inayo patikana ndani ya msitu wa amazon. Ndio
maana unaitwa mapafu ya dunia.
9. katika msitu wa amazon
kuna makabila zaidi ya 50 yana ishi hapo watu wameishi kwa maelfu ya miaka iliyo pita lakini watu hao wamekuja kuonekana miaka ya hivi
karibuni.
10. Green anaconda
Hawa ndio nyoka wakubwa zaidi duniani kwa sasa ni aina ya nyoka wanao patikana msitu wa amazon pekee wana rangi ya kijani na madoa meusi.
Hawa ndio nyoka wakubwa zaidi duniani kwa sasa ni aina ya nyoka wanao patikana msitu wa amazon pekee wana rangi ya kijani na madoa meusi.
11. Poison dork frog
Ni aina ya vyura wanaopatikana msitu wa amazon pekee wana sumu kali katika migongo yao mfano uchukue mwiba uchome ugongo wa chura hao kisha ujichome mwiba huo uvuki dakika kumi tunakua tusha kukosa
Ni aina ya vyura wanaopatikana msitu wa amazon pekee wana sumu kali katika migongo yao mfano uchukue mwiba uchome ugongo wa chura hao kisha ujichome mwiba huo uvuki dakika kumi tunakua tusha kukosa
12. American jaguar
Huyu anapatikana msitu wa amazon pekee. Ni mnyama jamii ya paka ila kafanana na duma licha ya kuwa ni mweusi mwili mzima kama kiwi, anapendelea sana kujificha juu ya miti mirefu ana uwezo mkubwa kuogelea, ni mnyama mwenye speed kali sana zaidi ya duma .

13. Harpy Eagle
Ni aina ya tai wanaopatikana msitu wa amazon hawa ni wakubwa zaidi hawa ni wapole wanaweza ishi na binadamu bila tatizo .
Ni aina ya tai wanaopatikana msitu wa amazon hawa ni wakubwa zaidi hawa ni wapole wanaweza ishi na binadamu bila tatizo .
14. Black caiman
Ni aina ya mamba wenye rangi nyeusi Hawa ni baadhi tu pia inasemekana nyoka mkubwa zaidi kuishi duniani aina ya titanoboa aliishi hapo Kizazi chake hakipo tena masalia ya nyoka huyo yanapatikana nchini colombia .

15. Mimea huitaji mwanga wa jua ili kustawi, ila msitu huu wa Amazon
unastaajabisha., mwanga wa jua unaopenya katika msitu ule ni mdogo sana lakini
bado mimea inastawi kwa kasi.
16. Asilimia kubwa ya madawa ya kisasa yanayotumika hospitalini
yanatokea katika mimea ya msitu wa Amazon. Na hadi sasa ni mimea asilimia moja
tu! Ambayo imetumika kutengeneza madawa.Bado kuna asilimia 99 haijatumika.
17. Vyakula vingi ambavyo tunakula vinatokana na mimea kutoka
Amazon! Mfano Ndizi, Pilipili nyeusi, Chocolate, kahawa, mahindi, mchele na
nyanya.
18. Takribani makabila hamsini ya watu wanaoishi katika msitu wa
Amazon hayajawahi kamwe kukutana na watu wanaoishi duniani!
19. Kuna
matunda takribani elfu tatu katika msitu wa Amazon. Ajabu sasa hadi sasa
matunda ambayo dunia imeyatumia ni matunda mia mbili tu. Wewe umekula mangapi
kati ya hayo mia mbili???

20. Ikiwa
msitu huo utaamuliwa kukatwa, basi utatoweka baada ya miaka arobaini. Yaani
itachukua miaka 40 kuisha.
21. Msitu
wa Amazon unasaidia kupunguza kasi ya ongezeko la joto. takribani asilimia 20
yahewa safi duniani huzalishwa kutoka kwenye msitu huo.
22. Kwa
mujibu washirika la kimazingira (WWF) Msitu wa AMAZONI unazalisha asilimia 20
ya maji safi duniani AMAZONI.
23. Inakaliwa
na viumbe zaidi ya milioni 3 wanyama na mimea pamoja na wakazi wa eneohilo ni
milion1asilimia 60 ya nchi ya PERU imefunikwa na mstu wa Amazon.
24. Kwa
mujibu wa Mamlaka za Brazil, inadaiwa mpaka sasa mioto 75,000 zimeteketeza msitu huo na jitihada
za kuuzima zinaendelea, moto mkubwa zaidi umewahi kutokea ndani ya Amazon mwaka
2013, lakini pia mwaka jana mioto 33,000 ziliteketeza msitu huo lakini huu wa
sasa unaonekana kutekeleza eneo kubwa zaidi!
25. Watu
wanaoishi kwenye mstu huu Amazon ni asili yao huko hawawezi toka hata
wakijengewa ma gorofa, pia ni kivutio kwa watalii kama wa, hadzabe huku
Tanzania na wamaasai.
26. Msitu
wa Amazon upo mbioni kupotea baada shughuri za kibinadamu kushamiri Sana
msituni apo. Katika ukataji miti , mashamba na n.k kwa mwaka hufikia sawa na
wiwanja 1200 vya mpira vinavyopotea.
27. Wakazi
wa msitu wa Amazoni huamini kwamba msitu huo umejaa nafsi zinazozurura usiku,
roho zinazosababisha magonjwa, na miungu inayojificha ndani ya mito ikisubiri
kuwanasa watu. Fikiria kuhusu Aguaruna, moja kati ya makabila makubwa zaidi
nchini Peru. Wanaabudu miungu mitano tofauti: “Baba Shujaa wa Vita,” “Baba wa
Maji,” “Mama wa Dunia,” “Baba wa Jua,” na “Baba wa uganga.” Wengi wanaamini
kwamba wanadamu wanabadilishwa kuwa mimea na wanyama. Kwa kuwa wanaogopa
kuwakasirisha viumbe wa roho, wenyeji huepuka kuwaua wanyama fulani nao
huwawinda wengine inapohitajika tu.
Waganga ndio husimamia maisha ya kidini na ya kijamii. Wao hutumia mimea kujipumbaza akili. Watu fulani katika maeneo hayo huwatazamia waganga hao watibu magonjwa, watabiri jinsi uwindaji na mavuno yatakavyokuwa, na kutabiri matukio ya wakati ujao.

28. Wakati
Msitu wa Amazon ukiongoza kwa ukubwa duniani unafuatiwa na msitu Congo Zaire wa
pili kwa ukubwa.
29. Ndani
ya Msitu wa Amazon Kuna mto mkubwa Sana unaoitwa Mto Amazon ambao ni wa pili
kwa Urefu duniani ukiacha Mto Nile unaoongoza duniani kwa Urefu.
30. Msitu
wa Amazon mapafu ya dunia kwani una faida nyingi Sana duniani. Kiafya,
kiuchumi, kijamii hata kimazingira.
Comments
Post a Comment