SEKTA
YA VIWANDA: KIINI CHA MAENDELEO TANZANIA
Sekta ya viwanda ina
nafasi kubwa ya kukuza uchumi wa Tanzania licha ya ukweli kwamba inakabiliwa na
changamoto nyingi Veneranda Sumila, Mwananchi Kwa mujibu wa aliyewahi kuwa Waziri
wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda: sekta ya viwanda ndiyo hasa
inayoshikilia ufunguo wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini kutokana na
uwezo wake wa kutengeneza ajira nyingi.
Akizungumza katika
uzinduzi wa ripoti ya sekta ya viwanda katika ukanda wa mashariki mwa Afrika,
Waziri Kigoda alisema sekta hiyo siyo tu injini ya taifa katika kukuza uchumi
bali pia katika kubadili maisha ya Watanzania. Ripoti hiyo ilikuwa inasisitiza
kuchochea matumizi ya teknolojia, uvumbuzi, uzalishaji pamoja na kuunganisha
viwanda na sekta nyingine za uchumi. Ripoti hiyo iliyozihusisha nchi za
Tanzania, Burundi, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Shelisheli na Uganda, ni sehemu ya
utafiti wa sekta ya viwanda uliyodhaminiwa na Kituo cha Rasilimali Ukanda wa
Mashariki mwa Afrika cha Benki ya Maendeleo ya Africa. “Kunaweza kuwa na nguzo
nyingine za maendeleo lakini hakuna hata moja yao inayoweza kushinda nguvu ya
viwanda.
Viwanda siyo tu
vinakuza uchumi kwa kuongezea bidhaa thamani bali pia vinatengeneza ajira
nyingi ambazo huongeza uzalishaji,” alisema Waziri Kigoda. Mkurugenzi mtendaji
wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) Godfrey Simbeye aliliambia gazeti la
Mwananchi katika mahojiano kwa njia ya simu kwamba nchi yoyote inayotaka
kujitegemea kwenye bajeti yake, lazima kwanza iimarishwe uuzaji wa bidhaa zake
zilizoongezewa thamani nje ya nchi. “Nchi inayotumia bidhaa za nje kwa wingi
kama Tanzania isitarajiwe kujitegemea kibajeti. Ili nchi yoyote iepuke misaada
ya kibajeti kutoka kwa wahisani, basi lazima iimarishe mauzo ya nje,” anasema
Simbeye.
Faida za
kuujenga uchumi wa viwanda
Uzalishaji
wa bidhaa katika viwanda umekuwa msingi muhimu wa mchakato wa utandawazi ambako
bidhaa nyingi zinazalishwa katika nchi fulani na kuuzwa kote duniani ilhali
vipuli vya kutengenezea bidhaa hizi tena zinatoka katika nchi tofauti.
Kila nchi
ina viwanda mbalimbali. Viwanda hivyo huisaidia nchi hiyo pindi iuzapo bidhaa
hizo, pia huisaidia nchi husika kunufaika kiuchumi kwa uwepo wa viwanda hivyo.
Viwanda
vina faida kubwa
sana katika nchi yenye viwanda hivyo; faida hizo ni:
·
Kuisaidia nchi
kukua kiuchumi,
·
Kupata fedha za kigeni,
·
Kulipa madeni wanayodaiwa,
·
Kuimarisha
huduma za jamii,
·
Kuajiri watu
ambao hawana kazi,
na
·
Kunufaisha taifa kwa ujumla
HEKO RAISI WETU JPM
Comments
Post a Comment