MAKALA: WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA ABIY AHMED ASHINDA TUZO YA NOBEL


HABARI ZA ULIMWENGU | 11.10.2019 | 15:00
Abiy Ahmed ashinda tuzo ya Nobel
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed ameshinda Tuzo ya Amani ya Nobel kutokana na juhudi zake za kuutatua mgogoro wa muda mrefu na nchi jirani Eritrea. Abiy ametunukiwa tuzo hiyo leo kwa kile Kamati ya Nobel imesema kuwa ni juhudi zake za kuleta amani na ushirikiano wa kimataifa. Tuzo hiyo inaonekana kumpiga jeki kiongozi huyo mwenye umri mdogo kabisa barani Afrika wakati akikabiliwa na mapigano ya jamii mbalimbali kabla ya uchaguzi wa bunge Mei 2020. Akizungumza na Kamati ya Nobel kwa njia ya simu baada ya kutangazwa mshindi, Abiy alisema ushindi wake ni habari nzuri kwa Adfrika, na hasa Afrika Mashariki na anatumai kuwa tuzo hiyo itaongeza kasi ya juhudi za amani ya kikanda. Tangu alipoingia madarakani Aprili 2018, Abiy mwenye umri wa miaka 43 ameweka sera ambazo zina uwezo wa kujenga jamii katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika na kuweka mazingira mapya mbali na mipaka ya nchi hiyo baada ya miaka mingi ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Comments