MUUNGANO
TANGANYIKA - ZANZIBAR 1964
Kwa ufupi
Mkataba wa Muungano ulitiwa saini na Mwalimu Julius
Nyerere na Abeid Amani Karume, Aprili 22, 1964, Zanzibar.
Ulithibitishwa na Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi Aprili 26, 1964, na Aprili 27, 1964 viongozi hao walikutana katika ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Dalaam kubadilishana hati za Muungano.
Sheria za Muungano ilitamka kwamba, Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar zililazimika, kuwa dola ya Jamhuri kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, jina ambalo lilibadilishwa Oktoba 28, 1964 na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitia sheria ya Jamhuri ya Muungano, sheria namba 61, ya mwaka 1964.

Msingi wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
ya mwaka 1977 na katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 ni Hati za Muungano za Mwaka
1964.
Hati za Muungano zilitiwa saini na Nyerere na
Karume, Aprili 22, 1964 na hapo Tanganyika na Zanzibar kuwa dola moja kwa
misngi inayotambulika kimataifa. Baada ya kuungana, Mwalimu Nyerere alikuwa
rais wa kwanza na Karume alikuwa makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Aprili 26, 1964, bunge la Tanganyika lilipitisha
sheria za Muungano, ambazo baadayezilithibitishwa na Baraza la Mapinduzi
Zanzibar.
Mnamo Aprili 27, 1964 waasisi wa Muungano
walibadilishana Hati za Muungano na wajumbe saba wa Baraza la Mapinduzi
waliapishwa kuwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Watanganyika na
Zanzibar ambao ni Amani Karume, Kassim Abdallah Hanga, Abdulrahman Babu, Hassan
Nassor Moyo, Aboud Jumbe, Hasnu Makame na Idris Abdul Wakil. Kati yao, Aboud
Jumbe na Hassan Nassor Moyo wangali hai.
Katiba ya muda ya mwaka 1965 ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania ilianisha mambo 11 ambayo yalikubalika kuwa ni ya Muungano ambayo
ni; Katiba na Serikali ya Muungano, Mambo ya nchi za nje, Ulinzi, Polisi,
Mamlaka juu ya mambo yanayohusika na hali ya hatari, Uraia, Uhamiaji, Mikopo na
Biashara za nje, Utumishi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Kodi ya
Mapato inayolipwa na watu binafsi na mashirika, ushuru wa forodha na ushuru wa
bidhaa zinazotengenezwa Tanzania unaosimamiwa na idara ya forodha, Bandari,
mambo yanayohusika na usafiri wa anga, posta na simu.
Katiba ya muda ya mwaka 1965 ilianisha utawala wa serikali ya mfumo wa chama kimoja, TANU kwa Bara na ASP kwa Zanzibar. Katiba hii, ilizingatia misingi ya makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964 na sheria za Muungano wa Tangayika za Zanzibar.

Katiba hiyo ilianisha serikali mbili, uwakilishi wa
Zanzibar katika bunge la Muungano ikiwa na mamlaka juu ya mambo yote ya
Muungano na mambo yasiyo ya Muungano kwa upande wa Tanganyika. Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar ikiwa na mamlaka juu ya mambo yote yasiyo ya Muungano
yahusuyo Zanzibar.
Hata hivyo mambo ya Muungano yaliongezwa kutoka 11 hadi 22 kutokana na mahitaji ya ndani ya nchi pamoja na mabadiliko yaliyokuwa yanaendelea kutokea ulimwengini baada ya Muungano.
Mwaka 1985, jambo la 12 linalohusu sarafu na fedha kwa ajili ya malipo na kurahisisha usimamizi wa fedha za kigeni na benki katika Jamhuri ya Muunagno wa Tanzania, liliingizwa.

Kufuatia kuundwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki
mwaka 1967, mambo matatu ya Muungano yaliyongezwa, ambayo ni leseni za viwanda
na takwimu; elimu ya juu; na usafirishaji wa anga.
Mwaka 1968, mambo ya maliasili ya mafuta, pamoja na mafuta yasiyochujwa ya magari na ama ya petroli na aina nyingine za mafuta au bidhaa na gesi asilia yaliyongezwa kwenye orodha hiyo.
Mwaka 1968, mambo ya maliasili ya mafuta, pamoja na mafuta yasiyochujwa ya magari na ama ya petroli na aina nyingine za mafuta au bidhaa na gesi asilia yaliyongezwa kwenye orodha hiyo.
Aidha mambo ya Muungano yaliendelea kuongezeka hadi
kufikia 21 kufuatia kuvunjika kwa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mwaka 1992 kufuatia mabadiliko ya mfumo wa siasa
nchini suala la 22 la uandikishaji wa vyama vya siasa na mambo mengine
yanayohusiana navyo liliongezwa kwenye orodha hiyo.
MJADALA KUHUSU MUUNGANO
Katika miaka hivi karibuni kumekuwa na mijadala
mbalimbali kuhusiana na muundo wa Muungano, baadhi wakitaka uwe wa zaidi ya
serikali mbili, wengine serikali moja, wapo wanaotaka Tanganyika iwe kivyake na
Zanzibar kivyake.
Hata hivyo hekima inaonyesha kwamba Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar unabaki kuwa ni fahari ya Watanzania, kwani mwelekeo wa
dunia katika nyanja mbalimbali, mataifa kuungana kwa ushirikiano wa aina
mbalimbali ni muhimu kuliko taifa moja kupambana kivyake.
Urejeaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya
kuvunjika mwaka 1977, uwepo wa SADC, ECOWAS, COMESA, na jumuiya nyingine nyingi
duniani kote, ni vielelezo kwamba ushirikiano baina ya mataifa ni suala
lisilohitaji mjadala.
Ieleweke kwamba hakuna ushirikiano usio kuwa na
matatizo kama ilivyo kwa Muungano wa Tanzania, vivyo hivyo muungano mwingine
kama vile ya United Kingdom (UK), Uingereza na United States of America (USA)
kwa maana ya Marekani na United Arabs Emirate (UAE), nayo ina matatizo, lakini
hata mara moja mjadala juu ya matatizo hayo siyo kuvunja ushirikiano bali
kutatua na wale wanaotaka kuvunja hushughulikiwa ipasavyo.
"Matatizo ya Muungano kama wa UK ni mabaya
zaidi, na hata UAE hawana ahueni, ila wanajua kwamba Muungano wao ni lazima.
Wamarekani wanapambana na watu wenye mawazo haya ya kuvunja miungano kwenye
majimbo ya Alaska, Hawaii na Texas na mwishowe wameamua kuweka kambi kubwa ya
jeshi la nchi kavu Texas; utitiri wa kambi za anga Alaska; na vituo vikubwa
kupindukia vya majini kule Hawaii. Hivi, hawa mabingwa wa demokrasia wanapoamua
kulinda nchi yao namna hii, unafikiri ni wajinga?
Walimwaga damu na waliyanunua majimbo haya na wamepitia shida kubwa, ndiyo maana leo wanajidai," anaandika mchangiaji katika mjadala kuhusu Muungano. Ni vyema Watanzania wakati huu wa kusheherekea miaka 48 ya Muungano, kila mmoja akajisikia ufahari wa kuwa na kitu kizuri kilichoasisiwa na Waafrika wenyewe na kudumu kwa umri huo.

Mawazo ya kubaguana kwa sababu zisizo na msingi,
pengine kukidhi matakwa na wakati kama vile ya kibinafsi na kisiasa, yasipewe
nafasi kuisambaratisha nchi. Chambilecho wahenga, umoja ni nguvu utengano ni
udhaifu.
Baada ya sherehe fupi ya kuurasimisha Muungano, siku iliyofuata
yaani Aprili 27, Rais wa Tanzania, Julius Nyerere alitangaza baraza lililokuwa
na mawaziri 23, huku watano wakitokea Zanzibar. Said Msawanya aliteuliwa kuwa
Waziri wa Kilimo, Misitu na Wanyama Pori; Jeremia Kasambala (Biashara na
Ushirika), Paul Bomani (Fedha), Oscar Kambona (Mambo ya Nje), Rashidi Kawawa
(Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa), na Tewa Said Tewa (Ardhi, Makazi na Maji).
Wengine ni Job Lusinde (Mambo ya Ndani), Kassim Hanga (Viwanda,
Madini na Nishati), Solomoni Eliufoo (Elimu), Dereck Bryceson (Afya), Michael
Kamaliza (Kazi), Sheikh Amri Abeid (Jamii na Maendeleo ya Utamaduni), Austin
Shaba (Serikali za Mitaa na Nyumba), Hassan Moyo (Sheria) na Abdul Idris Wakil
(Habari na Utalii).
STARZTZ: www.chuyangcustarah.over-blog.com
Comments
Post a Comment