Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania yatoa tahadhari juu
ya mvua kubwa
Thursday Oct 17th 2019
(GMT+08:00)
2019-10-05 17:17:12
Mamlaka
ya hali ya hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari kuwa mvua kubwa inatarajiwa
kunyesha leo katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Tanga na Zanzibar.
Taarifa
iliyotolewa na TMA imesema baadhi ya nyumba katika mikoa hii zitafunikwa
mafuriko, na shughuli za usafirishaji na biashara katika sehemu nyingine
zitaathiriwa sana.
Kuanzia
mwezi Mei mwaka huu mvua za mfululizo zimesababisha mafuriko makubwa jijini Dar
es salaam, na kusababisha familia zaidi ya elfu 1 kuhamishwa na kuharibu nyumba
zaidi ya 1500 na miundombinu muhimu. Mamlaka hiyo imesisitiza mahitaji ya
haraka ya kupunguza hatari ya mafuriko kupitia maendeleo endelevu.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO TAARIFA KWA UMMA
TAARIFA KWA UMMA
MAFURIKO JANGWANI KUPATIWA UFUMBUZI
Benki ya Dunia (WB) imekubali kushirikiana na Serikali ya Tanzania
katika kukabiliana na athari za mafuriko zinazosababishwa na mvua kubwa
zinazonyesha kila mwaka katika Jiji la Dar es Salaam na kuleta madhara makubwa
hususan katika eneo la Jangwani jijini humo. Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha
na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) wakati akizungumza na ujumbe wa
Benki ya Dunia ulioongozwa na Mkurugenzi wa Benki hiyo kwa nchi za Tanzania,
Somalia, Burundi na Malawi Bi. Bella Bird mjini Washngton. Dkt. Mpango amesema
kuwa Benki ya Dunia imekubali kusaidia kukabiliana na mafuriko katika bonde la
mto Msimbazi hasa katika eneo la kutoka Magomeni Mapipa kwenda Faya na tayari
Benki hiyo imeanza zoezi la kutafiti eneo la Jangwani ili kuweza kuangalia
namna nzuri ya kugharamia uboreshaji wa mifereji katika bonde la mto Msimbazi
pamoja na kuangalia kama kuna uwezekano wa kupata njia mbadala katika eneo hilo
ili kumaliza kero hiyo kwa wananchi wa Dar es Salaam. “Tumewaeleza Benki ya
Dunia changamoto hii ambayo imekuwa inajirudia kila mara na kusababisha upotevu
wa maisha ya watu, kusababisha kufungwa kwa barabara , watu kushindwa kwenda
kazini na wanafunzi kushindwa kwenda shule, hivyo wameonesha nia ya kumaliza
kero hii kwa wananchi “ Alisema Dkt. Mpango. Amesema kuwa baada ya timu ya
Benki ya Dunia kumaliza kufanya kazi yao kwa kushirikiana na Manispaa ya jiji
la Dar es Salaam, Serikali inaamini njia ya kudumu itapatikana na kuondokana na
tatizo hilo la mafuriko ya mara kwa mara katika eneo la Jangwani.
Imetolewa na ;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na
Mipango
Comments
Post a Comment