MWALIMU J. K. NYERERE NI MFANO BORA WA KUIGA KATIKA
KUWATETEA WA WANYONGE
Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, muasisi wa taifa la Tanzania
ataendelea kukumbukwa na wengi ndani na nje ya Tanzania, kwa kusimamia misingi
ya haki, amani, ustawi na maendeleo endelevu ya binadamu bila ubaguzi. Hata
Tanzania ya wakati huu, na Afrika katika ujumla wake, ina kiu kikubwa na watu
kama hawa wanaoweza kujitosa bila ya kujibakiza kwa ajili ya mafao ya wengi,
badala ya kujikita katika uchu wa mali, madaraka na utajiri wa haraka haraka na
kwamba uongozi ni huduma!
Familia ya Mungu nchini Tanzania kila mwaka ifikapo tarehe 14
Oktoba inafanya kumbu kumbu ya Siku ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,
alipofariki dunia nchini Uingereza kunako mwaka 1999. Ni kiongozi
aliyejipambanua kwa kujenga, kuimarisha na kutetea umoja wa taifa na muungano
wa watanzania. Alisimamia harakati za mapambano ya kisiasa na ukombozi ndani ya
Tanzania na kusini mwa Bara la Afrika. Alijitahidi kuimarisha mahusiano na
mafungamano ya kidiplomasia kati ya Tanzania na nchi jirani, kwa kuzingatia
misingi ya: haki, amani, utu na heshima ya binadamu.
Ni kiongozi aliyekazia maendeleo endelevu ya binadamu
yanayozingatia mahitaji yake msingi: kiroho na kiutu; kwa kukazia: haki msingi
za binadamu, utu na heshima yake na wala si maendeleo ya vitu, bali watu
wenyewe wapewe kipaumbele cha kwanza! Wadau wa kisiasa wanasema, Katiba Mpya si
kati ya vipaumbele vya Serikali ya awamu ya tano, lakini ni kati ya mahitaji na
changamoto kubwa zilizoachwa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa ajili ya
kujenga umoja, mshikamano na mafungamano ya watanzania katika medani mbali
mbali za maisha.
Kanisa mahalia bado linaendeleza mchakato wa Mtumishi wa Mungu,
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, mwamini mlei, Baba wa familia na kiongozi wa
kisiasa, ili siku moja, aweze kutangazwa kuwa Mwenyeheri na hatimaye Mtakatifu,
kama mfano bora wa kuigwa katika uwanja wa kisiasa aliyejitahidi kuhakikisha
kwamba, siasa kamwe haiwezi kuwa ni kikwazo katika ukuaji na ukomavu wake wa
maisha ya kiroho!
Historia fufi ya Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere
Alizaliwa (Butiama, mkoani Mara, pembezoni mwa Ziwa Nyanza, 13 Aprili 1922 - London, Uingereza, 14 Oktoba 1999)
alikuwa rais wa kwanza wa Tanzania, na mara nyingi anatajwa kama
"baba wa taifa". Kwa hakika aliiathiri kuliko yeyote yule.
Ndiye mwasisi wa itikadi ya ujamaa na kujitegemea iliyotangazwa
hasa katika Azimio la Arusha.
Kabla ya kuingia kwenye siasa alikuwa
ni mwalimu. Kazi hiyo
ndiyo iliyompatia jina ambalo lilimkaa maisha yake yote la "Mwalimu."
Kwanza aliongoza Tanganyika toka mwaka 1961 hadi 1964 kama waziri mkuu, halafu kama rais; baada ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, aliongoza Tanzania kuanzia
mwaka 1964 hadi mwaka 1985 kama
rais.
Mwalimu Nyerere ni kati ya viongozi
wachache wa Afrika ambao wameacha madaraka kwa hiari baada
ya kutawala kwa muda mrefu, akiwa bado anapendwa na wananchi walio wengi
katika nchi.
Alipostaafu urais mwaka 1985 alirudi kijijini kwake Butiama ambako aliendesha
shughuli za kilimo. Hata hivyo aliendelea kuwa na athari
kubwa katika siasa ya Tanzania hadi kifo chake.
Kwa ruhusa ya makao makuu ya Kanisa Katoliki duniani, Jimbo Katoliki la
Musoma linashughulikia kasi ya
kumtangaza mwenye heri na
hatimaye mtakatifu. Kwa sababu
hiyo anaitwa pia "mtumishi wa Mungu".
Maisha
yake
Julius Kambarage Nyerere alizaliwa
mwaka 1922 katika kijiji cha Butiama, wilaya ya Musoma, mkoa wa Mara, Tanzania (wakati ule: Tanganyika).
Alipokuwa mtoto Nyerere alichunga mifugo
ya baba yake; katika umri wa miaka 12
aliingia shule akitembea kilomita 30 hadi Musoma.
Baada ya kumaliza shule ya msingi aliendelea kusomea shule
ya wamisionari Wakatoliki huko Tabora.
Katika umri wa
miaka 20 alibatizwa akawa Mkristo Mkatoliki hadi mwisho wa maisha
yake.
Mapadri wakiona akili yake
kubwa walimsaidia kusomea ualimu huko Makerere, Kampala, Uganda kuanzia mwaka 1943 hadi 1945.
Akiwa Makerere alianzisha tawi la Umoja wa
Wanafunzi Watanganyika, pia alijihusisha na tawi la Tanganyika African Association (TAA).
Baada ya kumaliza masomo ya ualimu alirudi
Tabora akifundisha shule ya St.Mary.
Mwaka 1949 alipata skolashipu ya
kwenda kusoma kwenye Chuo Kikuu cha Edinburgh, Uskoti, Ufalme wa Muungano,
akapata M.A. ya historia na uchumi (alikuwa Mtanganyika wa kwanza
kusoma katika chuo kikuu cha Uingereza na wa pili kupata shahada ya elimu ya juu nje ya Tanganyika).
Aliporejea kutoka masomoni, alifundisha
Historia, Kiingereza na Kiswahili katika shule ya St. Francis iliyo
karibu na Dar es Salaam.
Mwaka 1953 alichaguliwa
kuwa rais wa chama cha Tanganyika African Association (TAA), chama ambacho
alikisaidia kukijenga alipokuwa mwanafunzi katika chuo kikuu cha Makerere.
Mwaka 1954 alibadilisha
jina la chama cha TAA kwenda chama cha Tanganyika
African National Union (TANU), ambacho pia kilikuwa cha kisiasa
zaidi kuliko TAA. Ndani ya mwaka mmoja chama cha TANU kikawa tayari chama cha
siasa kinachoongoza nchini Tanganyika.
Uwezo wa Nyerere uliwashtua viongozi
wa kikoloni akalazimika kuchagua kati ya
siasa na kazi ya ualimu. Nyerere alisikika akijisemea kuwa mwalimu kwa kuchagua
na mwanasiasa kwa bahati mbaya.
Alijiuzulu ualimu[1] na kuzunguka nchi nzima ya
Tanganyika kuzungumza na watu wa kawaida na machifu ili kuleta umoja katika
kupigania uhuru. Pia alizungumza kwa niaba ya TANU
katika Trusteeship Council na Fourth Committee ya Umoja wa Mataifa (UN) huko New York.
Uwezo wake wa kuongea na wa kuunganisha
watu ulimwezesha kufanikisha Tanganyika kupata uhuru bila umwagaji
wa damu.
Ushirikiano mzuri aliouonyesha
aliyekuwa gavana wa wakati huo, Richard
Turnbull, ulisaidia pia kuharakisha upatikanaji wa uhuru.
Mwaka 1961 Tanganyika
ilipata uhuru wake na tarehe 9 Desemba 1961 Nyerere alichaguliwa kuwa
waziri mkuu wa Tanganyika huru;
mwaka mmoja baadaye akawa rais wa kwanza wa Jamhuri ya Tanganyika.
Nyerere alikuwa kiungo muhimu katika
muungano wa Tanganyika na Zanzibar kutengeneza Tanzania mara baada ya mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964 yaliyomtoa
madarakani sultani wa Zanzibar Jamshid
bin Abdullah.
Julius Nyerere akiwa mzee mnamo mwaka 1977.
Tarehe 5 Februari 1977 aliongoza chama cha TANU
kuungana na chama
tawala cha Zanzibar Afro Shirazi Party na
kuanzisha chama kipya cha CCM (Chama cha Mapinduzi)
akiwa mwenyekiti wake wa kwanza.
Nyerere aliendelea kuongoza taifa hadi
1985 alipomwachia nafasi rais wa pili, Ali Hassan Mwinyi.
Aliacha kuongoza Tanzania ikiwa ni mojawapo
kati ya nchi maskini zaidi duniani, ingawa yenye huduma za elimu na afya
zilizoenea kwa wananchi wengi.
Hata hivyo aliendelea kuongoza CCM hadi
mwaka 1990 na kuwa na athari kubwa katika siasa
ya Tanzania hadi kifo chake.
Kwa mfano, inasadikika kuwa Nyerere
alishawishi uteuzi wa Benjamin
W. Mkapa kama mgombea
wa urais mwaka 1995, ambaye alichaguliwa
kuwa rais kwenye uchaguzi.
Nyerere alikaa muda mwingi kwake Butiama
akilima shamba lake. Pamoja na haya
alianzisha taasisi yenye jina lake; mwaka 1996 alionekana
akiwa mpatanishi wa
pande mbalimbali za vita vya
wenyewe kwa wenyewe huko Burundi.
Tarehe 14 Oktoba 1999 aliaga dunia
katika hospitali ya St Thomas mjini London baada ya kupambana na kansa ya damu.
Mafanikio
Nyerere
akichanganya udongo wa Zanzibar na Tanganyika wakati
wa muungano mwaka 1964.
Kati ya mafanikio makubwa ya Nyerere kuna:
kujenga umoja wa taifa kati ya watu wa makabila na dini tofauti, na hivyo
kudumisha amani ya muda mrefu tofauti na hali
ya nchi jirani, iliyofanya Tanzania iitwe
"kisiwa cha amani".
Pia kustawisha utamaduni wa Kiafrika pamoja na lugha ya Kiswahili, kushinda ubaguzi wa rangi, kutetea usalama
wa taifa katika vita dhidi
ya mvamizi Idi Amin wa
Uganda.
Kutoa mchango kwa vyama vya ukombozi vya nchi za Kusini mwa Afrika kama vile: Zimbabwe (ZANU), Afrika Kusini (ANC na PAC), Namibia (SWAPO), Angola (MPLA)
na Msumbiji (Frelimo).
Ukosoaji
dhidi yake
Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere
Nyerere analaumiwa kwa siasa yake ya kiujamaa
kuwa ilichelewesha maendeleo ya
kiuchumi wa Tanzania. Siasa yake ya ujamaa ilishindikana kwa kiasi kikubwa
baada ya mwaka 1976 kwa sababu mbalimbali za nje na za
ndani ya nchi.
Baada ya kuona kuwa uchumi wa Tanzania
hautaweza kusimama kwa siasa ya kijamaa na kuwa hataweza kuvumilia kuendesha
nchi kwa siasa nyingine ambazo yeye hakuwa na imani nazo, Nyerere kwa hiari
yake mwenyewe aliamua kustaafu nafasi ya urais kuanzia uchaguzi wa mwaka 1985
na kumwachia usukani Ali
Hassan Mwinyi, aliyetawala kwa siasa ya uchumi wa soko huria.
Katika hali ya kukubali ukweli, Nyerere katika tafrija ya
kumwaga alitamka juu ya siasa yake upande wa uchumi: “Nimefeli. Tukubali
hivyo.”
Kosa lingine ambalo wengine wanaona Nyerere
alilifanya ni kumhadaa aliyekuwa Rais wa Zanzibar Mzee Abeid
Amaan Karume kwa kuziunganisha Tanganyika na Zanzibar, na
kuanza kupora mamlaka ya Zanzibar
kidogokidogo. Kwa hivi sasa Wanzanzibari wengi wamechoka na Muungano huo, na
wanataka uhuru wa nchi yao ili wapumue. Hata upande wa bara wananchi
wengi wanalalamikia kutoweka kwa Tanganyika na serikali yake.
Pia kuna makundi ya Waislamu wanaomtuhumu kwa kuendesha kwa
siri vita dhidi ya dini yao na kupendelea Wakristo katika utoaji wa elimu na
madaraka,japo wasomi wengi kwa kipindi cha utawala wake walikuwa Wakristo.
Sifa zake
Nyerere
akicheza bao kwake Butiama, akitazamwa na mwandamizi wake katika
urais Ali Hassan Mwini, mke wake Mama Maria,
na kaka yake, chifu Burito.
Pamoja na hayo, Nyerere bado anakumbukwa na
Watanzania hasa wa hali ya chini kutokana na sera zake
za kujali utu. Pia ataendelea kukumbukwa na Waafrika
barani kote hasa kwa mchango wake mkubwa wakati wa harakati za kupigania uhuru
katika nchi mbali mbali barani Afrika.
Ni mmoja wa viongozi wachache waadilifu
waliokwepa kujilimbikizia mali pamoja na kutawala
kwa miaka zaidi ya 24.
Kaburi la Nyerere kijijini Butiama.
Mwishoni mwa maisha yake Nyerere aliishi
kama mkulima wa kawaida kijijini kwake Butiama. Alipatwa na kansa ya
damu (leukemia) akafariki Uingereza wakati wa kutibiwa katika
mji wa London tarehe 14 Oktoba 1999.
Alizikwa mahali pa kuzaliwa kwake, kijiji
cha Butiama.
Heshima
na Tuzo
Nishani
Nishani
|
Nchi
|
Mwaka
|
Ref
|
|
Nishani ya José Marti
|
1975
|
|||
Nishani ya Tai ya Kiazteki (Ukosi)
|
1975
|
|||
Nishani ya Amílcar Cabral
|
1976
|
|||
Nishani ya Eduardo Mondlane
|
1983
|
|||
Nishani ya Agostinho Neto
|
1985
|
|||
Nishani ya Masahaba wa O. R. Tambo (Dhahabu)
|
2004
|
|||
Nishani ya Kifalme cha Munhumutapa
|
2005
|
|||
Nishani Ubora wa Lulu ya Afrika (Bwana tukufu)
|
2005
|
|||
Nishani ya Katonga
|
2005
|
|||
Medali ya Ukombozi wa Kitaifa
|
2009
|
|||
Medali ya Kampeni Dhidi ya Mauaji ya Kimbari
|
2009
|
|||
Nishani ya Kikale cha Welwitschia Mirabilis
|
2010
|
|||
Nishani ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
|
2011
|
|||
Nishani ya Kitaifa cha Burundi
|
2012
|
|||
Nishani ya Jamaika
|
Tuzo
·
1982: the
Third World Prize
·
1983: Nansen
Refugee Award
·
1986:
Sir Seretse
Khama SADC Medal
·
1987: Lenin
Peace Prize
·
1988: Joliot-Curie Medal
of Peace
·
1995: Gandhi
Peace Prize
Kisha kufa
·
2000:
Statesman of the 20th century by the Chama cha Mapinduzi
·
2009: World
Hero of Social Justice by the 63rd President of UNGA, Miguel
d'Escoto Brockmann[13]
·
2011: Tanzania
Professional Network Award[14]
Machapisho
ya mwl.Julius K. Nyerere
·
Freedom and
Unity (Uhuru
na Umoja): Mkusanyiko wa maandiko na hotuba, 1952–1965 (Oxford
University Press, 1967)
·
Freedom and
Socialism (Uhuru
na Ujamaa). Mkusanyiko wa maandiko na hotuba, 1965-1967 (1968)
o
Ndamo zimo:
"The Arusha Declaration"; "Education for self-reliance";
"The varied paths to socialism"; "The purpose is man"; and
"Socialism and development."
·
Freedom &
Development (Uhuru
na Maendeleo). Mkusanyiko wa maandiko na hotuba, 1968-73 (Oxford
University Press, 1974)
o
Ndani zimo
mada za elimu kwa watu wazima; uhuru na maendeleo; kujitegemea; na miaka kumi
ya uhuru.
·
Ujamaa -
Essays on Socialism' (1977)
·
Crusade for
Liberation (1979)
Comments
Post a Comment