RAISI WA NIGERIA AFUATA NYAYO ZA RAISI MAGUFULI
Katika kudhibiti
matumizi mabovu ya fedha ya umma, mheshimiwa raisi Muhamad Buhari wa Nigeria
kafuata nyayo za mheshimiwa raisi wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania katika
kudhibiti safari za nje ya nchi zisizo na tija kwa taifa hilo kubwa barani
Afrika. Hii imeonekana kuwa ni njia mojawapo ya kupunguza matumizi yasiyo ya
lazima ili hela nyingi ielekezwe kwenye miradi ya maendeleo ya nchi kwa ustawi
wa maisha ya wananchi wote wa jamhuri ya shirikisho ya Nigeria.
Hii
inadhihirisha kuwa ili kuwa na Afrika tuitakayo kadri ya mpango wa Umoja wa
Afrika (AU) uliopo sasa wa 2063, Afrika inahitaji viongozi kama raisi John Pombe Josefu Magufuli wenye uzalendo
na wenye uthubutu wa kufanya maamuzi magumu kwa maslahi mapana ya mataifa yao.
Ama kweli raisi Magufuli ni kioo cha bara la Afrika kwa sasa. Mungu amzidishie
neema na baraka raisi Magufuli wa Tanzania.
Na Mgata
Albogasto
albogasto.mgata@gmail.com
Comments
Post a Comment