Rais Magufuli atangaza kuhamia
Dodoma rasmi

Rais wa Tanzania , John Pombe Magufuli ametangaza kuhamia rasmi
katika mji mkuu wa taifa hilo, Dodoma.
Rais Magufuli anakuwa rais wa kwanza kati ya marais watano
waliotawala nchi hiyo , kutekeleza uhamisha wa makao makuu ya Tanzania kutoka
jiji la kibiashara la Dar es Salaam kwenda Dodoma.
Uhamisho wa makao makuu ya serikali mkoani Dodoma, umechukua
safari ya zaidi ya miaka 42 iliyopita.
Rais Magufuli alitoa amri ya serikali kuhamia Dodoma mwezi Julai
2016 wakati alipopewa wadhifa wa mwenyekiti wa chama tawala, Chama Cha
Mapinduzi.
Ambapo waziri mkuu alianza kuhamia katika mji huo na kufuatia na
viongozi wengine pamoja na wizara tangu mwaka 2016.

Magufuli alidhihirisha hilo hapo jana ,12.10.2019 kwa
kujiandikisha katika katika daftari la orodha ya wapiga kura katika kijiji cha
Chamwino mkoani Dodoma.
Chamwino ni eneo ambalo, ikulu mpya ya rais iko.
Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa alihamia rasmi mji wa
Dodoma septemba 26, 2016.
Umbali wa mji wa Dar es Salaam mpaka Dodoma ni takribani
kilomita 450.
Kwa muda wa miezi minne sasa ofisi za serikali zimekuwa
zikihamishwa kwenda mji wa Dodoma.
Tangazo la Rais Magufuli la kuhamishia serikali Dodoma ilikuwa
na mtazamo tofauti tofauti , wengi wakiwa na hofu juu ya shughuli za na familia
zao.
Huku wenjeji ikiwa fursa kwao na kuibua msisimko mpya na
matumaini kwa wafanyabiashara.
Majumba makubwa na ya kifahari yanaendelea kujengwa katika mji
huo.

Lakini changamoto kubwa ya mabadiliko hayo bado ikiwa ni kwa
watumishi wa umma ambao inawabidi kufunga safari kila wakati kwa ajili ya
familia zao.
Aidha wengi kuona mpango huu umeathiri familia zaidi katika ndoa
na maendeleo binafsi.
Huduma muhimu za afya na shule , bado wananchi wana matumaini
sekta nyingi binafsi zitaamia katika mji huo.
Dodoma ulitangazwa kuwa mji mkuu wa Tanzania na mwasisi wa taifa
hilo mwalimu Julius Nyerere mwaka 1973.

Sanamu la Mwalimu Nyerere lililopo mjini Dodoma limekuwa kuvutio
kikubwa mjini humo hasa kwa vijana na wageni ambao mara nyingi huenda kupiga
picha za ukumbusho
Comments
Post a Comment