MAKALA: YAJUE MENGI KUHUSU MLIMA KILIMANJARO


IJUE HISTORIA YA MLIMA KILIMANJARO NA ASILI YAKE
Mlima Kilimanjaro unavyoonekana kutoka Moshi

Kilimanjaro ni mlima wenye volcano na  mrefu kuliko yote barani Afrika. Mlima huu uko nchini Tanzania katika Mkoa wa Kilimanjaro . Una urefu wa mita 5,895 ( futi 19,340).
Kilele cha Kibo kwenye mlima Kilimanjaro Hali halisi Kilimanjaro ni zaidi ya mlima tu, ni kama safu ndogo ya milima mitatu: Kibo, Mawenzi na Shira. Hii mitatu inaonekana kama vilele vitatu vya mlima mmoja hivyo si vibaya kusema Kilimanjaro ni mlima.

Kilimanjaro ni volkeno iliyolala kwa sasa. Kwenye kilele cha Kibo gesi bado inatoka. Kumbukumbu ya wenyeji ina habari ya mlipuko mnamo mwaka 1730 . Kilele cha juu cha Kibo kinaitwa Uhuru. Mtu wa kwanza wa kufika kileleni hapo alikuwa Johannes Kinyala Lauwo kutoka Marangu aliyewaongoza Wajerumani Hans Meyer na Ludwig Purtscheller tarehe 6 Oktoba 1889 wakati wa ukoloni wa Ujerumani. Wakati ule waliita ncha ya juu "Kaiser-Wilhelm-Spitze" (kwa Kijerumani: Kilele cha Kaisari Wilhelm) kwa heshima ya Kaisari wa Ujerumani. Kibo ina theluji na barafuto ndogo kadhaa.


HISTORIA YA JINA
Ramani ya 1888 inayoonyesha jina " Kilima-Ndscharo " katika Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Asili ya jina "Kilimanjaro" haijulikani kikamilifu. Vyanzo vya kimaandishi vinajulikana tangu takriban mwaka 1860 ambako wapelelezi wazungu walitumia jina hili katika taarifa zao wakidai "Kilimanjaro" ilikuwa jina la Kiswahili . Pamoja na umbo hili kulikuwa pia na tahajia ya sehemu mbili ama "Kilima-Njaro" au kwa namna ya Kijerumani “Kilima-Ndscharo”.

Johann Ludwig Krapf aliandika mnamo 1860 kuwa Waswahili kwenye pwani waliita mlima huu "Kilimanjaro". Alisema pia ya kwamba hao Waswahili walieleza maana yake kuwa ama “mlima mkubwa” au “mlima wa misafara” ingawa mwenyewe hakukubali maelezo haya. Kwa elezo la mwisho "Kilima" kilimaanisha "mlima" na "Jaro" labda "misafara".

Jim Thompson aliandika mnamo 1885 kuwa jina Kilima-Njaro lilichukuliwa mara nyingi kuwa na maana ya "mlima mkubwa" lakini mwenyewe alipendelea maeelzo tofauti  yaliyosema "mlima mweupe" "Njaro" ni Kiswahili cha Zamani kwa "ng’ara". Vizvo hivzo Krapf aliandika ya kwamba aliwahi kuwatembela Wakamba mnamo 1849 walioita mlima “Kima jaJeu” yaani mlima mweupe [5] Leo hii Wakamba wangesema “Kiima Kyeu” na elezo hili limekubaliwa na watafiti mbalimbali.

Wengine huona ya kwamba ni wazungu wasiojua Kiswahili vema waliochanganya “mlima” na “Kilima”.

Wengine wamejaribu kuona msingi wa jina katika lugha ya Kichagga. Hapa wanadai uwezekano kuwa "Kileman" imetokana na neon la Kichagaa "kileme" inayomaanisha “kinachoshinda” au neno "kilelema" inayomaanisha "kilichokuwa vigumu, kilichoshindikana".

Katika hoja hili "Jaro" imetokana na Kichagga “njaare” (aina ya ndege, au kufuatana na wengine chui) au kutoka neno “jyaro” (msafara). Elezo nyingine ni ya kwamba Wachagga walisema mlima huu ni hauwezi kupandwa "kilemanjaare" au "kilemajyaro" na wapakazi au wafasiri kutoka pwani waliichukua kuwa jina la mlima na kutafsiri vile kwa wazungu.
Mlima Kilimanjaro ukitokea katikati ya mawingu.

Tangu miaka ya 1880 mlima umekuwa sehemu ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani ukaitwa "Kilima-Ndscharo" kwa Kijerumani. Tarehe 6 Oktoba 1889 Hans Meyer alikuwa mtu wa kwanza anayejulkikana kupanda mlima na kufika hadi kilele cha Kibo. Alichagua jina la "Kaiser-Wilhelm-Spitze" ("Ncha ya Kaisari Wilhelm". That name apparently was used until Tanzania was formed in 1964,  when the summit was renamed "Uhuru", meaning "Freedom Peak" in Kiswahili.

JIOLOJIA YA MLIMA  NA  TABIA  ZA KIJOGRAFIA
Kilimanjaro inapanda hadi mita 4877 juu ya tambarare karibu na mji wa Moshi uliopo miguuni pake. Hii inafanya kilele chake kuwa mita 5895 juu ya uwiano wa bahari. Kilimanjaro ni volkeno ya rusu iliyojengwa na rusu za majivu , zaha na mata nyingine. Ni volkeno ndefu kuliko zote duniani nje ya Amerika Kusini.


Vilele vitatu vya kivolkeno juu ya Kilimanjaro ni:

·         Kibo iliyo juu zaidi
·         Mawenzi yenye kimo cha mita 5149
·         Shira yenye urefu wa mita 4005.

Mawenzi na Shira ni volkeno zilizozimika lakini Kibo ni volkeno ya kulala inaweza kuwaka tena. Uhuru Peak ni sehemu ya juu kwenye ukingo wa kasoko la Kibo.

Taasisi ya Tanzania National Parks Authority [16] na UNESCO vinataja kimo cha Uhuru Peak kuwa mita 5895. Kipimo hiki kimetokana na upimaji wakati wa ukoloni wa Uingereza mwaka 1952 . Tangu upimaji ule kimo cha mlima kimepimwa tena: kinaonyesha kuwa mlima unapungua polepole. Kipimo kilikuwa mita 5892 mwaka 1999 na mita 5891 mwaka 2014.

Muundo wa ndani wa Kilimanjaro haujulikani sana kwa sababu hadi sasa haujatokea mmomonyoko mkubwa unaoweza kufunulia ndani yake.
Kilele cha Kibo kilivyoonekana kutoka angani mwaka 1938.

BARAFU  na BARAFUTO 
Mlima Kilimanjaro hujulikana kuwa ni mlima wa Afrika wenye kofia ya barafu ya kudumu. Pamoja na Kilimanjaro kuna sehemu mbili nyingine tu barani Afrika, ni Ruwenzori na Mlima Kenya. Lakini kiasi cha barafu imepungua kwa kipindi cha zaidi ya miaka 100. Mwingereza P.C. Spink aliona mwaka 1944 ya kwamba barafu ilipungua sana kulingana na taarifa aliyojua kutoka mpandaji wa kwanza Hans Meyer. Baina 1912 eneo la ngao ya barafu limepungua kutoka kilomita za mraba 12 hadi 1.85 km² kwenye mwaka 2009. Hii inalingana na kupunguzwa asilimia 85%. Sababu kuu ya mabadiliko haya ni kupungukiwa kwa kiwango cha usimbishaji katika mazingira ya mlima tangu mwisho wa karne ya 19.

Maana Kilimanjaro ni mlima wa juu vile ya kwamba mvua zote pamoja na ukungu na usimbishaji mwingine unaofika kwenye kilele chake utaganda na kuwa theluji. Theluji inayokaa muda mrefu tena katika ganda nene itakuwa barafu. Lakini wakati uleule mishale ya jua zinasababisha kupotea kwa theluji na barafu kwa njia ya uvukizaji . Kwa jumla kuongezeka au kupungukiwa kwa barafu kwenye kimo hiki ni swali la kiasi cha mvua na usimbishaji mwingine zinazofika hapa.

Leo hii kuna barafuto kwenye Kibo pekee pamoja na mabaki ya ngao ya barafu kwenye tambarare ya kilele na kwenye mitelemko ya Kibo. Hii ngao ya barafu bado iko kwa sababu Kilimanjaro ni mlima usio na vilele vikali unaofika juu ya kimo cha mstari wa jeledi . Kasoko ya Kibo imepita na kukata ngao hiyo. 5 Siku hizi hakuna miendo ya maana inayoonekana kwenye barafuto za kilele kwa sababu unene wao imepungua mno.. Utafiti wa kijiolojia umeonyesha ya kwamba kulikuwa na vipindi vitano vya upanuzi wa barafuto katika miaka 500,000 iliyopita vilivyofuatwa na vipindi vya kupungua.

Ngao ya barafu mfululizo ilifunika mlima wote hadi kimo cha mita 3,200 miaka 24,000 – 25,000 iliyopita wakati barafuto kote duniani zilienea sana. Kuna dalili ya kwamba barafu yote mlimani iliwahi kupotea kabisa takriban miaka 11,500 iliyopita kutokana na
ukame dunaini wakati ule. Kuongezeka kwa usimbishaji wakati wa Holoseni (miaka 11,500 iliyopita) kumeruhusu kurudi kwa barafu mlimani. Barafuto ziliweza kudumisha kipindi cha ukame miaka 4,000 iliyopita.

Wakati wa kutembelewa mara ya kwanza katika miaka ya 1880, kilele cha Kibo kilifunikwa kabisa kwa ngao ya barafu yenye eneo la kilomita za mraba 20 hivi na mikondo ya barafuto iliendelea wenye mitelemko ya kando. Isipokuwa pia ya kati, kaldera yote ilifunikwa na barafu. 

UOTO KATIKA MLIMA KILIMANJARO 

Kuna misitu asilia zinazofunika takriban kilomita ya mraba 1,000 kwenze mlima. Sehemu ya chini hulimwa kwa kupanda mahindi, maharagwe na alizeti , pia ngano upande wa magharibi. Kuna mabaki ya uoto wa savana ya awali yenye miti kama Acacia , Combretum , Terminalia na Grewia. Kuanzia kimo cha mita 1000 hadi mita 1800 kuna kilimo cha kahawa kwa namna ya kidesturi ya "Wachaga inayopanda miti na mazao kwa pamoja. Uoto asilia umebaki pekee katika mabonde majkali yasiyoweza kutumiwa kwa kilimo na hapa ni tofauti na uoto kwenye maeneo ya juu zaidi.

Kuanzia kimo cha mita 1000 hadi mita 1800 kuna kilimo cha kahawa kwa namna ya kidesturi ya " Wachaga inayopanda miti na mazao kwa pamoja. Uoto asilia umebaki pekee katika mabonde majkali yasiyoweza kutumiwa kwa kilimo na hapa ni tofauti na uoto kwenye maeneo ya juu Zaidi.

Kwenye mitelemko ya kusini penye mvua nyingi kuna misitu ya mvua yenye miti aina ya Ocotea usambarensis pamoja na kangaga na epipythi . Juu zaidi penye ukungu wa kudumu kuna Podocarpus latifolius , Hagenia abyssinica na Erica excelsa pamoja na kuvumwani.

Upande wa kaskazini ulio kavu zaidi pana misitu ya mizeituni, Croton - Mlungu-mbago (Calodendrum), Cassipourea (Mugome na Msikundazi) na Juniperus (Mtarakwa) kadri kimo kinaongezeka.

Juu zaidi kati ya mita 3,100 na 3,900 hufuata kanda la vichaka vya Erica (mdamba ) na juu yake kunamajanimajani tu kama Helichrysum hadi mita 4500.

Utafiti kwenye kasoko ya Maundi kwenye kimo cha mita 2780 umeonyesha ya kwamba uoto wa Kilimanjaro ulibadilika katika mwendo wa karne na milenia. Wakati wa baridi kwenye enzi ya barafu miaka 42,000 – 30,000 iliyopita misitu ilishuka chini na kanda la mdamba lilitokea takriban mita 1,500 chini ya hali yake ya sasa. 

WANYAMA WANAOPATIKA MLIMA KILIMANJARO 

Hakuna wanyama wakubwa wengi waliobaki mlimani. Wanyama wengi Wanapatikana hasa kwenye misitu na sehemu za chini ya mlima. Tembo na nyati wanaweza kuwa na hatari kwa watalii wanaopanda mlima na pia kwa wakulima. Pongo, vinyonga , digidigi , paa, Nguchiro , nyani mbalimbali kama mbega , komba, chui , chozi na ngiri wametazamiwa pia. Punda milia na fisi wamepatiokana mara chache kweye tambarare juu ya Shira. 

Kuna spishi chache zinazopatikana Kilimanjaro pekee hizi ni pamoja na “kirukanjia wa Kilimanjaro”  na spishi ya kinyonga kinachoitwa Kinyongia tavetana. 

Comments