_________________________________________________________
Kifaransa
Kifaransa (kwa Kifaransa: français) ni lugha
ya Ufaransa (pamoja na maeneo
yake ya ng'ambo), Ubelgiji ya Kusini, Uswisi ya Magharibi, Luxemburg na Kanada. Inazungumzwa pia katika nchi
nyingi za Afrika kama vile Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo, Senegal, Mali, Shelisheli, Chad, n.k., Asia ya Kusini na Amerika zilizokuwa koloni za Ufaransa.
Wasemaji
Takwimu kuhusu matumizi ya Kifaransa hutofautiana.
Kadirio ndogo lasema kuna watu milioni 87 wanaotumia Kifaransa kama lugha ya
kwanza, na tena milioni 100 wanaoitumia kama lugha ya pili. Kadirio kubwa
lataja milioni 112,6 wasemaji wa lugha ya kwanza pamoja na milioni 60,6 wenye
uwezo wa kutumia Kifaransa karibu kama lugha ya Mama. Halafu hutajwa takriban
milioni 100 -110 wanaotumia Kifaransa kikazi, kibiashara au masomoni jumla
takriban milioni 300 wasemaji wa Kifaransa duniani.
Historia ya lugha
Kifaransa ni kati ya lugha za Kirumi. Asili yake ni Kilatini lugha ya Waroma wa Kale. Hadi mwaka 50 KK watu
waliokalia Gallia (eneo la Ufaransa wa leo)
walitumia lugha mbalimbali za Kikelti.
Baada ya uvamizi na Waroma Gallia ilikuwa sehemu ya Dola la Roma. Lugha ya Kilatini ilienea
hadi kuwa lugha ya watu wengi. Kikelti kimebaki hadi leo katika maeneo madogo
kama Ubritani.
Kilatini hiki jinsi kilivyojadiliwa na watu wa kawaida
katika Gallia kilipokea kiasi cha maneno na matamshi na lugha ya Kikelti. Baada
ya mwisho wa Dola la Roma lugha iliendelea kubadilika haraka zaidi. Makabila
ya Kigermanik walivamia Gallia na kuleta
athira ya lugha zao.
Haya yote yaliunda lugha ya Kifaransa ambayo ni lugha
karibu sana na Kilatini hivyo pia na lugha kama Kiitalia, Kihispania na Kireno.
Kifaransa kilichokuwa rasmi kilifuata lahaja ya eneo
la Paris. Tangu 1634 kuna Akademia ya Kifaransa aabayo ni taasisi ya kulinda usafi
wa lugha.
Kifaransa kilienea kimataifa kwa sababu Ufaransa ilikuwa
taifa lenye maendeleo mengi katika Ualya. Kifaransa kilikuwa katika nchi nyingi
lugha ya elimu na pia ya mawasiliano ya kimataifa jinsi ilivyo siku hizi
Kiiingereza mahali pengi.
Baada ya Ufaransa kuwa nchi yenye koloni lugha ilisambazwa hata nje ya
Ulaya. Ubelgiji yenye Kifaransa kama lugha rasmi ilikuwa pia na koloni na
kupeleka lugha huko.
Hali ya Lugha kimataifa
Kifaransa ni lugha ya kitaifa, lugha rasmi, lugha ya utawala au lugha ya mawasiliano katika nchi zifuatazo:
·
Monaco
·
Lugha ya kitaifa pamoja na lugha nyingine
Uswisi (lugha
rasmi hasa katika mikoa ya magharibi)
·
Lugha rasmi kimkoa
Italia katika
mkoa wa Val
d'Aoste
Lugha rasmi ya nchi zifuatazo
1. Benin
2. Burkina Faso
3. Burundi
5. Chad
6. Komori
10. Guinea
11. Guinea ya Ikweta
12. Madagaska
13. Mali
14. Niger
15. Rwanda
16. Senegal
17. Shelisheli
18. Togo
·
Lugha ya utawala:
·
Lugha ya elimu na mawasiliano, lakini wala lugha ya
kitaifa wala lugha rasmi katika
·
Lugha rasmi ya Vanuatu
·
Lugha ya mawasiliano na elimu katika Siria, Kambodia, Vietnam, sehemu za India (Pondicherry, Mahé, Karikal na Yanaon) *Lugha ya
kitaifa na lugha rasmi katika maeneo
ya kifaransa ya Polynesia
ya Kifaransa na Kaledonia Mpya
·
Lugha rasmi ya Haiti
·
Lugha ya utawala katika Jamhuri ya
Dominika
·
Moja ya lugha mbili za kitaifa katika Kanada; ni lugha rasmi ya pekee katika jimbo
la Quebec (13% ya Wakanada wote hujua
Kifaransa pekee, 18% wanajua lugha zote mbili)
·
Lugha ya kitaifa na lugha rasmi katika maeneo
ya kifaransa ya Guyana ya
Kifaransa, Guadeloupe, Martinique na Saint-Pierre
na Miquelon.
Comments
Post a Comment