MAKALA: TETESI ZA SOKA ULAYA

Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 19.11.2019: Neymar, Benitez, Willian, Pochettino, Enrique, Pogba, Guardiola, Fernandes, Berge

NeymarHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionNeymar alijiunga na PSJ mwaka 2017 na ameshinda mataji mawili na mabingwa hao wa Ufaransa
Mchezaji nyota wa Brazil Neymar, 27, amekataa kusaini upya mkataba wake na klabu ya Paris St-Germain, ambao unamalizika mwaka 2022. (Sport)
West Ham huenda ikamgeukia Rafael Benitez ikiwa wataamua kuachana na Manuel Pellegrini. (Mirror)
Kiungo wa kati wa Chelsea na Brazil Willian, 31, hana mpango wa kukubali ofa ya kurefusha mkataba wake kwa miaka miwili msimu huu ili apate nafasi ya kujiunga na Barcelona. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania)
WillianHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKiungo wa kati wa Chelsea na Brazil Willian, 31, anapania kujiunga na Barcelona
Mauricio Pochettino amefanya mazungumzo na mwenyekiti Daniel Levy kuhusu hatama yake katika klabu ya Tottenham. (Telegraph)
Shirikisho la soka la Uhispania limempatia Luis Enrique, ofa ya kurejea tena katika timu ya taifa kama mkufunzi wake. (AS)
Kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 26, angelipendelea kurejea Juventus kuliko Real Madrid. (Tuttosport - in Italian)
Paul PogbaHaki miliki ya pichaGOOGLE
Image captionPaul Pogba,angelipendelea kurejea Juventus kuliko Real Madrid
Ajenti wa Pep Guardiola hajafutilia mbali uwezekano wa mkufunzi huyo wa Manchester City boss kurejea Bayern Munich hivi karibuni. (AS)
Manchester United huenda ikamsajili kiungo wa kati wa Ureno Bruno Fernandes, 25, mwezi Januari huku Sporting Lisbon ikiripotiwa kuwa inahitaji kukusanya fedha za kulipa deni la karibu £57m. (O Jogo - in Portuguese)
Chelsea inamfuatilia kiungo wa kati wa Genk raia wa Norway Sander Berge, 21, ambaye pia ananyatiwa na Liverpool na Napoli. (Goal.com)
Bruno FernandesHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionManchester United huenda ikamsajili kiungo wa kati wa Ureno Bruno Fernandes
Juventus na Inter Milan zimeonesha nia ya kutaka kumnunua beki wa Manchester United na England Chris Smalling, 29, ambaye kwa sasa yuko Roma kwa mkopo. (Sun via Corriere della Sera)
West Brom inatafakari kumuuza mlinzi wa England wa chini ya miaka -20 Nathan Ferguson, mwezi Januari ikiwa nyota huyo wa miaka 19- hatakubali kurefusha mkataba wake wa sasa ambao unakamilika msimu ujao. (Express and Star)
Arsenal inapanga kuwatuma wasaka talanta wakekumchunguzakiungo wa kati wa Red Bull Salzburg na Hungary Dominik Szoboszlai,19. (Football Insider)
Nathan FergusonHaki miliki ya pichaREX FEATURES
Image captionWest Brom inatafakari kumuuza mlinzi wa England wa chini ya miaka -20 Nathan Ferguson
Ajenti wa mshambuliaji wa Wolves,Patrick Cutrone amepuuzilia mbali tetesi kuwa kiungo huyo wa Italia wa miaka 21 huenda akaondoka Molineux. (Samp News - in Italian)
Leeds iko tayari kumuuza beki wake mwingereza Lewie Coyle, 21, ambaye kwa sasa anachezea kwa mkopo Fleetwood, mwezi Januari. (Football Insider)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii

Comments