Mvua yaua watatu
Iringa
MONDAY JANUARY 27 2020
Kwa ufupi
By Berdina Majinge,
Mwananchi bmajinge@mwananchi.co.tz
Watu watatu wamekufa huku kaya 62 zikikosa makazi kutokana na
mafuriko yaliyokikumba kijiji cha Tungamalenga na Idodi wilayani Iringa Mkoa wa
Iringa. Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Januari 27, 2020 mkuu
wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela amesema wamekufa watu watatu, wakiwemo
watoto wawili. Amesema watoto hao nyumba wanayoishi ilizingirwa na maji, wakati
wakitoka nje mama yao alishika mti na hakusombwa na maji.
“Watoto hawakushika mti wakasombwa na maji, mwili wa mtoto mmoja
na mtu mwingine tumeipata, wamezikwa ila tunaendelea kutafuta mwili wa mtoto
mwingine,” amesema Kasesela. Mkuu huyo wa Wilaya amesema eneo la Pawaga nyumba
takribani 41 zimebomoka na nyingine za tarafa ya Idodi zimeathiriwa na mvua kwa
kiasi kikubwa. “Niwashukuru wenyeviti wa vijiji hivyo kwa kuwaunganisha
wananchi waliokumbwa na mafuriko na kuwaweka katika nyumba ambazo
hazijazingirwa na maji,” amesema Kasesela, akibainisha kuwa barabara
inayounganisha Hifadhi ya Taifa Ruaha kupitia Msembe Tungamalenga haipitiki.
Huyu ndiye Mkuu wa Wilaya ya Iringa ndugu Richard Kasesela akiwa katika eneo la Mafuriko...
Comments
Post a Comment