MAKALA: MLIPUKO WA UGONJWA WA CORONA



VIRUSI VYA CORONA
Virusi vya Corona (kwa Kiingereza: Coronavirus) ni kundi la virusi vinavyoweza kusababisha magonjwa kwa wanyama (mamalia na ndege) lakini pia kwa binadamu[1]. Inaaminiwa ni aina ya virusi vilivyohama kutoka kwa wanyama na kuathiri binadamu pia.
Virusi vya Corona vipo vya aina mbalimbali, zikiwemo 229E, NL63, OC43, HKU1 na SARS-Cov-2 
Tabia za pamoja
Virusi vya corona huwa na uwezo wa kubadilika na aina nyingi husababisha magonjwa yasiyo hatari sana upande wa binadamu. Kudhoofika kwa mwili kutokana na mashambulio ya virusi kunafungua milango kwa bakteria wabaya kukuvamia na kusababisha maambukizo ya mfumo wa upumuo, kama mafua au homa ya mafua (influenza), yanayoishia kwa kawaida baada ya siku kadhaa, lakini kuna pia maambukizo ya hatari kama nimonia inayoweza kusababisha kifo. Hivyo inatakiwa watu wapunguze kutumia kwa pamoja vitu hatarishi kama vile vya ncha kali[4].
Hadi sasa hakuna chanjo au dawa ya kudhibiti virusi vya aina hii. Kwa hiyo uponyaji hutegemea mara kwa mara nguvu ya kinga mwilini cha kila mtu. Hii inamaanisha virusi hivi huleta hatari hasa kwa watu wenye kinga cha mwili kilichodhoofishwa.
Aina hizo za virusi zina uwezo wa kubadilika, miaka ya nyuma ulikuwa na mabadiliko kadhaa yaliyosababisha vifo vya watu na kuenea haraka kimataifa, hivyo kusababisha hofu za epidemiki au hata pandemia.
SARS
SARS (Severe acute respiratory syndrome) ulikuwa ugonjwa sugu wa mfumo wa upumuo uliosababishwa na virusi vya corona aina ya SARS-CoV. Uliripotiwa mara ya kwanza huko Asia kwenye Februari 2003 ukaendelea kusambaa katika miezi iliyofuata katika nchi zaidi ya 20 katika AmerikaUlaya na Asia hadi kwisha. Ugonjwa ulianza kuonekana kwa homa juu ya  38, maumivu ya kichwa na kujisika dhaifu. Asilimia 10-20 za wagonjwa walihara. Wengi walioambukizwa waliendelea hata kupata nimonia. Kulikuwa na taarifa za watu 8,098 walioambukizwa, na 774 walifariki katika nchi 17[5], wengi wao nchini China. SARS haijatokea tena tangu mwaka 2004.
Covid-19 (2019 Novel Coronavirus SARS-Cov-2)
Mwisho wa mwaka 2019 lilitokea badiliko jipya la virusi vya corona lililotambuliwa mara ya kwanza mjini WuhanChina. Serikali ya China inalaumiwa kwa kujaribu kuficha ugunduzi huo kwa maagizo yalitolewa tarehe 2 Januari 2020.
Aina hiyo ya virusi vya corona iliitwa mwanzoni 2019 Novel Coronavirus (2019-nCoV) na hatimaye ikapewa jina la SARS-Cov-2, na ugonjwa unaosababishwa nayo Covid-19. Usambazaji wake ulionekana kuanza kutokana na virusi vya wanyama vilivyofikia binadamu. Magonjwa ya aina hiyo huitwa zuonosia (zoonotic disease).
Wagonjwa walionyesha matatizo kwenye njia ya upumuo; wengine waliathiriwa kidogo tu, lakini wengine waligonjeka vibaya hadi kufa. Dalili zilizotambuliwa hadi mwisho wa Januari 2020 ni pamoja na homa, kukohoa na ugumu wa kuvuta pumzi. Inaonekana dalili za ugonjwa zinaweza kuanza takriban siku 2 hadi 14 baada ya kuambukizwa. Walio hatarini zaidi ni watu waliodhoofishwa na magonjwa mengine au wenye mfumo dhaifu wa kinga mwilini kwa sababu nyingine, kwa mfano umri mkubwa.
Hadi mwisho wa Januari 2020 takriban watu 10,000 waliambukizwa, idadi ya vifo ilikuwa mnamo 200. Virusi vilienea hadi nchi nyingine kwa njia ya abiria wa ndege za kimataifa. Wakazi wa Wuhan na miji mingine ya China yenye wagonjwa wamekataliwa kuondoka kwao baada ya hali ya karantini kutangazwa.
Katikati ya Februari 2020 maswali mengi kuhusu virusi hivi vilibaki bila jibu, lakini Shirika la Afya Duniani lilitoa tathmini kuwa
·         zaidi ya asilimia 80 za wagonjwa huonekana kuwa na ugonjwa mwepesi, wanapona
·         kati ya asilimia za wagonjwa kuna maambukizi mazito yanayosababisha matatizo ya kupumua, hata nimonia, na asilimia 15 kudai walazwe hospitalini
·         takriban asilimia 5 huwa na magonjwa hatari
·         mnamo asilimia 2 hufa; hatari ya kifo inapatikana hasa kwa wazee, kuna mfano michache ya watoto
·         utafiti wa ziada bado unahitajika
·         kuna dalili kwamba virusi vya Covid-19 vinaweza kudumu hadi siku 8 kwenye uso wa kitu kilichoguswa na mgonjwa na bado kusababisha maambukizi

Uenezi wa Covid-19 nje ya China
Katika Februari 2019 virusi viliendelea kuenea nje ya China, kupitia watu waliosafiri baina ya China na nchi nyingine. Tabia ya virusi kutosababisha ugonjwa mkali kwa wengi ilikuwa msingi kwa uenezaji usiotambuliwa mwanzoni hadi kufikia watu waliogonjeka vibaya. Milipuko ya kwanza ilionekana katika IranKorea Kusini na Italia ambako serikali zilitangaza hali ya karantini kwa maeneo kadhaa. Kufikia mwisho wa mwezi huo, wagonjwa wa nchi nyingine wamezidi wale wa China.
Mwisho wa Februari wataalamu walianza kujadiliana kama hii ni pandemia, yaani epidemia (mlipuko) katika nchi nyingi za dunia.
Ushauri wa kujikinga dhidi ya maambukizi
Maambukizi husambaa hasa kwa majimaji ya mwilini, kama matone madogo ya mate au chafya; mtu aliyeambukizwa atakuwa na virusi kwenye mikono yake akigusa pua au mdomo. Inawezekana mtu aliyeambukizwa asionyeshe dalili za ugonjwa bado lakini anaweza kupitisha virusi tayari.
Unashauriwa:
·         kunawa mikono mara kwa mara kwa angalau sekunde 20 kwa maji na sabuni. Ukiwa nayo tumia dawa yenye alikoholi (si chini ya asilimia 60) kusafisha mikono.
·         usiguse macho, pua na midomo kwa mikono kama hujanawa
·         epuka kuwa karibu sana na wagonjwa, tumia barakoa ya kinga ukimhudumia mgonjwa
·         ikiwezekana epuka kuingia katika msongamano mkubwa wa watu maana wenye virusi hawaonekani kirahisi.
·         kaa nyumbani ukiwa mgonjwa (ugonjwa wowote - maana kinga yako ni dhaifu katika hali hii)
·         tembea na karatasi za shashi (kama huna, hata karatasi ya choo / toilet paper) uitumie ukikohoa au kupiga chafya, halafu uitupe mahali pa takataka
·         safisha mara kwa mara vitu unavyovigusa (vikiwa pamoja na kikombemezadawatisimu yako)
Tanbihi
5 million people left Wuhan before China quarantined the city to contain the coronavirus outbreak, taarifa ya gazeti Business Insider USA, kupitia www.pulselive.co.ke, tarehe 27-01-2020
Coronavirus | About | Symptoms and Diagnosis | CDC (en-us). www.cdc.gov (2020-01-25). Iliwekwa mnamo 2020-01-28.
Coronavirus (en). WebMD. Iliwekwa mnamo 2020-01-28.
Coronavirus (en). www.who.int. Iliwekwa mnamo 2020-03-09.
COVID-19: WHO renames deadly coronavirus, tovuti ya Al-Jazeera ya 11-2-2020
Julia Naftulin, Business Insider. Wuhan Coronavirus Can Be Infectious Before People Show Symptoms, Official Claims (en-gb). ScienceAlert. Iliwekwa mnamo 2020-01-28.
Ongezeko la baktria wasiosikia dawa. Iliwekwa mnamo 2020-03-09.
Smith, Richard D (2006). "Responding to global infectious disease outbreaks: Lessons from SARS on the role of risk perception, communication and management". Social Science & Medicine 63 (12): 3113–23. doi:10.1016/j.socscimed.2006.08.004 . PMID 16978751 .


Comments